EN Anza mradi

04Studio

Studio ya ubunifuyenye mizizi Dar es Salaam

Karibu Legendary Studios. Tunaamini kwamba tunachokichagua huunda tabia zetu, nazo tabia hizo hutuunda sisi. Na yote hayo yanaanzia kwenye sanaa moja ambayo mara nyingi tunaisahau: sanaa ya ubunifu.

Magomeni Apartments

Magomeni Apartments

Hadithi yetu

Legendary Studios ni studio ya usanifu majengo na ubunifu wa ndani iliyoko Dar es Salaam. Tunabuni nyumba, ofisi, maduka, migahawa, hoteli na zaidi kote Tanzania. Kila mradi tunaufanya kwa moyo wote na kwa umakini, ili upate muundo wa kifahari ulioundwa mahsusi kwa ajili yako. Na kila mradi unakuja na 3D halisi, uione kabla ya kujenga.

Studio ilianzishwa na Fredrick Makunja, na inashirikiana na timu ya kuaminika: msanifu majengo aliyesajiliwa na AQRB anayeandaa na kusaini ramani za kibali, wahandisi wa structure, wakadiriaji majenzi (QS) na mafundi wanaogeuza michoro kuwa majengo halisi.

Fredrick Makunja
Mwanzilishi na mbunifu mkuu

01Misingi yetu

Tunasikiliza kwanza

Kila mradi huanza na wewe: jinsi unavyoishi au unavyofanya kazi, kiwanja chako na bajeti yako. Mtindo unafuata baadaye.

Tunabuni kwa bajeti halisi

Tunachagua vifaa na mbinu zinazofaa hali ya hewa yetu na fedha ulizonazo, na tunaboresha muundo wakati wa kupanga bajeti, si baada ya kuanza ujenzi.

Unaona kabla ya kujenga

3D halisi inakuwezesha kuitembelea nafasi yako na kubadili mawazo wakati mabadiliko bado hayajakugharimu hata shilingi moja site.

02Tunaoshirikiana nao

  • Msanifu majengo mshirika aliyesajiliwa na AQRB kwa ramani za kibali
  • Wahandisi wa structure, umeme na maji
  • Wakadiriaji majenzi (QS) kwa BOQ
  • Mafundi, maseremala na wasambazaji wa kuaminika

03Zana zetu za kazi

ArchiCADSketchUp3ds MaxCoronaV-RayD5 RenderLumionBlenderAutoCAD

Vipimo hadi milimita: kila mchoro huanza na vipimo halisi vya site.

04Jinsi tunavyofanya kazi

  1. 01

    Tunasikiliza

    Tunakutana site au kwa video. Tunakusikiliza: jinsi unavyoishi au unavyofanya kazi, kiwanja chako na bajeti yako.

  2. 02

    Tunapima

    Tunapima na kupiga picha za kiwanja au nafasi, ili kila mchoro uanze na vipimo halisi.

  3. 03

    Tunachora

    Mipangilio na machaguo ya awali. Wewe unachagua mwelekeo kabla hatujaingia kwenye undani.

  4. 04

    Tunakuonyesha kwa 3D

    Picha halisi za 3D za nafasi yako. Unaitembelea na kuomba mabadiliko wakati kubadili bado ni nafuu.

  5. 05

    Tunajenga

    Ramani za mwisho, orodha za vifaa na, ukipenda, tunasimamia site hadi siku ya kukabidhi.

Karibu

Tusimulie ndoto ya nafasi yako.

Tutumie picha chache, mchoro au hata wazo tu. Tutakujibu ndani ya siku moja ya kazi, pamoja na hatua zinazofuata na mwongozo wa gharama.

Tuchati WhatsApp